MTOTO wa siku moja mnamo Mei 24, mwaka huu ameokotwa katika makaburi ya Vingunguti, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya mfuko wa rambo.
Taarifa zilizopatikana katika eneo la tukio zilidai kuwa, mtoto huyo alisikika akilia na wasamaria ambao siku hiyo usiku walienda na kumkuta akiwa katika mfuko mweusi huku mbwa wakimnyemelea.
Mtoto huyo wa kike baada ya kuokolewa na wasamaria wema alipelekwa kwenye kituo cha afya kiitwacho Afya Bora ambapo wafanyakazi wake, Catherine Shayo na Magreth Masanja walimpa huduma ya kwanza kisha wakatoa taarifa Kituo cha Polisi Buguruni na kupewa kumbukumbu namba BUG /RB/6238/2012.
Baadaye mtoto huyo mchanga alipelekwa katika Hospitali ya Amana na PC Nel.
Uchunguzi unaonesha kwamba, maeneo ya Buguruni na Vingunguti yanaongoza kwa utupaji watoto ambapo Aprili 27 na Mei 4, mwaka huu watoto wawili waliokotwa mmoja akiwa amefariki.
Na Makongoro Oging'
Global Publisher
Note: Jamani wadada mpaka lini tabia hii, mbona tunakua wanyama hivi? yani inasikitisha kwa kweli.
Kwa nini mnafanya ngono zembe halafu hamtaki kukubali matokeo? Walaaniwe wote wanaotoa mimba au kutupa vichanga kama hivi,karne hii si ya kupata mimba za bahati mbaya, kuna njia za kila aina za uzazi wa mpango ili kuzuia mimba zisizotarajiwa zinazoleta maafa kama haya. Kuna watu wanalia usiku na mchana kuomba Mungu wapate watoto wakati wengine mwawatupa.
Ole wenu wenye tabia hizo damu za hawa watoto zitawaandama siku zote za maisha yenu.
Nimeumia sana.
Majoy.
inaumiza sana, hii ni roho ya kinyama
ReplyDeleteYani inaumiza kwa kweli watoto wasio na hatia kuteseka kwa dhambi ya wazazi wao.wanawake hatukutakiwa kabisa kuwa na roho mbaya hivi.
ReplyDelete