WAIGIZAJI Mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jacob Stephen ‘JB’ na Aunty Ezekiel wamechaguliwa kuwa mabalozi wa channel ya Zuku Swahili movie channel itakayokuwa ikirusha filamu zinazotumia lugha ya Kiswahili, sehemu kubwa ya filamu hizo zitakuwa ni zile zilizosambazwa na kampuni ya Steps ya jijini Dar es Salaam alisema mkurugenzi wa Zuku kwa upande wa Tanzania Johnson.
“JB na Aunty Ezekiel wamepata nafasi ya kuwa mabalozi wa Zuku Swahili movie kwa Tanzania, hii ni hatua moja mbele kwa maendeleo ya filamu Swahiliwood, lakini ni furaha kwa wasanii wenyewe kwa Zuku kuwachagua kuwa mabalozi wa channel inayoonyesha kazi zao za filamu, lakini pia Zuku inakusudia kukuza lugha ya Kiswahili kwa kupitia channel hiyo,”anasema Johnson.
Zuku kwa kushirikiana na Steps Entertainment ndio wanaosimamia channel hiyo kwa ushirikiano na mtayarishaji mkuu akiwa ni ni kampuni ya Steps, channel ya Zuku Swahili movie itaonyesha filamu za kimapenzi, mapigano, Kwaya, Vichekesho na makala pia, uzinduzi rasmi wa Zuku Swahili movie utafanyika mwezi wa nane,
channel hiyo utaiona kwa
kupitia king’amuzi cha Zuku.
channel hiyo utaiona kwa
kupitia king’amuzi cha Zuku.
Johnson amewaomba watanzania wanaopenda filamu za Kitanzania kuitumia channel hiyo itakapozinduliwa kwani watapata burudani ya kutosha kupitia channel hiyo iliyokusudia kutoa elimu na burudani kwa wapenzi wa filamu, Komedi, Kwaya, na makala pia.
STORY NA PICHA KWA HISANI YA FILAMUCENTAL BLOG(SWAHILI HOOD PORTAL)
No comments:
Post a Comment
Thank you for your comment