Social Icons

Friday, October 28, 2011

BAADHI YA NJIA YA KUZIKABILI STRESS ZA MAISHA

Katika Maisha tunapitia mambo mengi sana ambayo kwa namna moja au nyingine hufanya maisha kuvutia au sometimes kukarahisha, Hii ni hali ya kawaida kwa Binadamu hivyo basi yabidi kukubaliana nayo coz hizo ni just 'ups' n 'downs' katika maisha ila chamsingi ni kutokata tamaa na daima kusonga mbele. Kero za maisha(stress) husababishwa na mambo mengi sana ikiwemo Ugumu wa maisha,kazi, mapenzi,Familia,Masomo n.k

Ungana nami Edo Daniel (pichani hapo juu) kujua baadhi ya MAMBO MUHIMU yanayoweza kukuongoza kupambana na hizi kero za maisha(stress) ni kama zifuatazo:-

1. UGUMU WA MAISHA
Hili ni tatizo kubwa Duniani kote hivyo basi haina haja ya kujipa stress kama maisha yamekua magumu kwako basi ndiyo mwisho wa kila kitu cha msingi ni kuweza kumiliki ulivyonavyo kinachotutesa wengi wetu ni kutaka mambo makubwa wakati uwezo ni mdogo. Yanini ukakope ili kuweka heshima mtaani au kujifanya unakula burger daily wkt kipato chako ni cha chini?
Kua simple fanya vitu vya uwezo wako hapo daima utaenjoy chamsingi ni kua na malengo ya maisha yako si vyema kuishi maisha kwa kuiga wengine mana hujui njia walizopitia. Pia ni muhimu kuweka akiba kwa ajili ya mabadiliko yoyote katika maisha kumbuka leo unafanya kazi au unapata pesa lakini ipo siku unaweza ukafukuzwa kazi au hutopewa tena pesa so yabidi kujiandaa kwa kipindi kama hicho.
Remember Self Commitment is what matters in everything you do.

2. KAZI
Kazi halali humfanya mtu kua na amani moyoni hata kwa mwenyezi Mungu hivyo ni muhimu kufanya kazi kwa bidii.Kazi pia humfanya mtu kuheshimika machoni pa wengine hata kama ukipatacho ni kidogo. Ikumbukwe kuna watu wengi sana wako mitaani wakitafuta kazi hivyo ni muhimu kumshukuru Mungu kama wewe ni kati ya wateule wake. Ukiwa kazini mambo mengi hutokea kama kukwaruzana na Bosi au wafanyakazi wengine lkn hiyo haipaswi kukunyima raha au kukukatisha tamaa kwani daima binadamu hatuko sawa na hiyo ilishawahi kuwatokea watu wengi sana duniani so usijione kama 'jumba bovu limekuangukia'.

Ukiwa katika foleni tazama nje utakuta ombaomba wengi hao hawakupenda kua ombaomba wala hawakuzaliwa hivyo so tutunze kazi zetu na kuzipenda pia.
kwa wale ambao bado wanatafuta kazi msikate tamaa yaweza kupita muda mrefu usipate kazi hiyo yaweza kua ni somo ambalo umepewa ili utakapopata kazi uweze kuithamini, chamsingi ni kusali na kumwomba Mungu katika yote uyapitiayo.
Remember PRAYER is an essential element in human survival.

3. MAPENZI
"Mapenzi yana run dunia" ni kati ya misemo maarufu duniani kuhusu mapenzi. Kiukweli uchaguzi wa nani uwe nae ni muhimu sana katika kukuondolea stress maishani trust me kama ukichemka hapa ndo umechemka maishani na utabaki na stress milele so what should you do? Kwanza ni kujitahidi kua na mpenzi mmoja ambae moyo wako umeridhia kua nae mtu ambae ukiwa nae unajickia faraja,mtu ambae mnaendana kifikra na kiimani ikumbukwe " Love is the spiritual relationship" so spiritually muwe mnaendana kwani kwa kufanya hivyo itapunguza stress ktk maisha mana hakutakua na kupingana katika maamuzi ya nini kifanyike muda gani.
Stress nyingi huletwa na watu kua na wapenzi wengi na kudhani kama wanapata 'Total satisfaction' huko ni kujidanganya hakuna jipya unalolipata kwa kua na wapenzi tofauti tofauti zaidi ya magonjwa na kuzidisha stress. 'Kama huridhishwi na unachokipata zungumza na umpendae ukupatie ili maisha yaendelee'.Pia ni muhimu kutokua na rush katika swala la ndoa kwani ni muhimu sio kukimbilia kuoa bali ni kua na uhakika na huyo unaempa maisha yako awe mwenza wako. Muhimu pia kumshirikisha Mungu katika uchaguzi wako wa nani uwe nae kwani mume au mke mwema anatoka kwa Mungu.

4.FAMILIA
Familia ni kiungo muhimu kinachoweza kukuongezea au kukupunguzia stress hivyo basi familia inabidi ichukuliwe kwa makini sana. Familia yatakiwa iwepo kukusuport na kukushauri lakini usikubali familia kukuharibia mipango na malengo yako. Ni vizuri kusaidia mambo ya kifamilia lakini kamwe usiruhusu mambo hayo yachukue kila furaha uliyonayo maishani.
Yani kama unao uwezo wa kusaidia ni vizuri ukasaidia itakupa baraka kwa Mungu na kwa yule umsaidiae. Lkn kamwe msaada usizidi uwezo.Ikiwezekana hata waweza kuwapotezea wanafamilia in the process of making good life mana mwisho wa yote utabaki wewe kama mama/baba wa familia na hao wengine watakua na familia zao.
Vivyo hivyo hata kwa marafiki pia kama unaona hawakusaidii lolote let them go.

5. MASOMO
Kusoma kwa bidii na kuzingatia kinachokufanya usome ni njia nzuri ya kuepukana na stress zinazosababishwa na kufail mitihani au kupanic wakat mitihani ikikaribia.
Hakuna uchawi katika masomo ni kwamba tunatakiwa tu kuweka fikra zetu na muda wetu kusoma mambo mengi ili kuepukana na stress za sup na failures ktk masomo.

Najua kuna mambo mengi ambayo ukiyafanya waweza kua stess free man/woman chamsingi ni KUTHAMINI ZAIDI MAISHA YAKO NA KUYACHULIA KAMA NDO KILA KTU KWAKO. Ukitaka chukua ukiona haikusaidii achana nayo mana hizi sio fomula.



Shukrani kwa  Edo Daniel.......

2 comments:

  1. hahahahahahahaha Joy thanx a lot my dear nimefurahi kwa kukubaliana na mawazo yangu

    ReplyDelete
  2. a wiseman's article.
    keep it up Edo

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...