Social Icons

Friday, November 4, 2011

UVAEJE UNAPOKWENDA KWENYE USAILI(INTERVIEW)


Nimeshawahi kuona mtu akikosa kazi kisa tu alichovaa hakiendani kabisa na kazi anayoiomba.kazi ilikua ni ya uhasibu halafu bidada kapiga suruali ya jinsi shati lake ndo hizi sikuhizi wanaida 'kimodo' make up usoni ka katuni .Tatizo linakuja hapa kwamba hakuvaa kulingana na alivyotakiwa avae ukizingatia kuwa wahasibu wengi siku zote wako smart hata asipovaa tai lakini atavaa shati na suruali yake safi kabisa na hata kama atavaa jinsi na shati basi atatupia na koti kwa juu hii ni kwa wote wanawake au wanaume na sisi wanawake jamani tuwe tunaangalia make up za kupaka unapokwenda ofisini nitazungumzia hilo siku zijazo.

Wataalamu wanasema unapoingia kwenye interview muonekano wako peke yake unatosha kujua kama unafaa au hufai kwa post hiyo.
Soma hapa chini nimekosa wa kutafsiri.....
''First impressions are formed in 7 seconds.  38% of a first impression is based on inflection and tone of voice (how you say things), 7% is based on what you actually say, and a whopping 55% of a first impression comes from NONVERBAL cues!  In short, more than half of every first impression is based on how you look!''
Haya sasa tuangalie ni jinsi gani au mavazi gani utatakiwa uvae kwa baadhi ya kazi kama picha zitakavyoonesha hapa chini:-

Conservative Industries – Accounting, Finance, Law, Consulting, etc. :


Creative Industries – Advertising, Graphic Design, Music, etc. :

Fashion Industry
Haya baada ya kujivalia zako hivyo utakua poa ila kuna vitu muhimu vya kuzingatia na ni muhimu sana kufuta kama nitakavyosema hapa chini kama utaona itakufaa kwa manufaa yako mwenyewe:-
DOs
  • Nywele zako ziwe safi na uzi-style vizuri sio kujiziba uso
  • Poda kidogo ili kuondoa mng'aro wa mafuta usoni
  • Mascara
  • Lip gloss kidogo au kwa mbali so domo ling'ae kama umekula kitumbua
  • Wanja kwa mbali
DONTs 
  • Fanya kinyume na vyote hivyo hapo juu mf. usiwe na nywele chafu na ambazo hazijawekwa kwa style nzuri
  • Usijipake make-up nyingi usoni hasa poda ili usionekane kituko.n.k 

4 comments:

  1. yani nimecheka hapa eti sio domo ling"ae km umekula kitumbua hahaha mwenyewe busy kwenye usajili na domo lako hahaha asante majoy

    ReplyDelete
  2. dah...asante sana majoy blog.. kwa kweli hili ni somo zuri mno..endelea kutujuza viewers wako. asante, mdau, mikocheni.

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...