Social Icons

Tuesday, May 15, 2012

MGOMBA BARABARANI.............!!!

Mgomba uliopandwa katikati ya barabara.

Baadhi ya magari yakipata kwa kupishana baada ya mgomba huo kupandwa barabarani.

UNAWEZA kuona kama ni kitendo cha utani lakini ni moja ya kuwakilisha ujumbe kwa wizara husika ya Ujenzi ambayo inaongozwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli.

Leo asubuhi kuliibuka usumbufu katika barabara ya Mwananyamala hospitali baada ya mtu mmoja kupanda mgomba katikati ya barabara hiyo jirani kabisa na geti la kuingilia hospitalini humo, yote kuonyesha serikali kuwa ni jinsi gani barabara hiyo muhimu ilivyokuwa mbovu.

Akiongea na mtandao huu mwanamke mmoja ambaye alikutwa akiushangaa mgomba huo alisema kuwa kupandwa kwa mgomba katikati ya barabara ni sahihi kabisa kwani serikali haijali barabara hiyo.

“Aliyefanya hivi kanifurahisha sana kwani kila siku barabara hii inapigiwa kelele lakini wahusika wanadharau,” alisema mwanamke huyo.

(PICHA / HABARI NA SHAKOOR JONGO /GPL)

 

4 comments:

  1. hahahahhaha wamewakomesha lol, maana serikali nao wanafumbia macho sana vitu muhimu kama barabara

    ReplyDelete
  2. Yani huyo aliyefanya ubunifu huo wa kupanda mgomba barabarani kanifurahisha sana maana wakiuona huo mgomba na shimo wataliona hahahaaa!!!

    ReplyDelete
  3. KWIKWIKWIKWIIIII WATZ TUPO JUU YANI MGOMBA BARABARANI. MWEEE

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...