Social Icons

Monday, June 18, 2012

JAMANI TUMUOMBEENI MZEE SMALLDUA za Watanzania zinahitajika kumuombea msanii aliyepata umaarufu Bongo kupitia sanaa ya uigizaji wa vichekesho, Said Ngamba maarufu kama Mzee Small (pichani), Risasi Jumamosi linakupa habari za kina.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana hivi karibuni kutoka kwa ndugu mmoja wa karibu (hakutaka kutajwa jina), zinasema kuwa afya ya msanii huyo aliyewahi kutamba katika vikundi vingi vya maigizo bado ni tete.
Hivi karibuni Mzee Small aliripotiwa kuugua ugonjwa wa kiharusi na kulazwa katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar kabla ya kuhamishiwa katika  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Pamoja na kwamba  ameruhusiwa kutoka Muhimbili lakini hali ya Mzee Small bado siyo nzuri,” alisema ndugu huyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya madaktari wa Muhimbili, awali Mzee Small alitibiwa shinikizo la damu ili kudhibiti tatizo la kiharusi ‘stroke’ na kupata nafuu kiasi.

“Baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali, hivi sasa familia imeamua kumhamishia Mzee Small kwa mwanaye mkubwa anayeishi Gongo la Mboto ili aweze kupata nafasi ya kufanya mazoezi na kupumzika,” alisema ndugu huyo na kusisitiza kuwa nguvu zaidi zinahitajika ili kuweza kumtibu msanii huyo.

Chanzo:Erick Evarist na Gladness Mallya
Global Publishers.

No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...