Social Icons

Monday, September 10, 2012

MAMA TERESA


Miaka 15 iliyopita tarehe 5 Septemba,1997,

Mmoja kati ya watu muhimu katika Karne ya 20 alifariki Dunia. Jina lake aliitwa Agnes Gonxha Bojaxhiu japokua duniani alijulikana kama MAMA TERESA.

Alizaliwa Macedonia Mwaka 1910 na kujiunga na na 
shirika la masista wa Loreto na baadae kuhamia India alikokua akifanya kazi ya ualimu wa shule. 
Mwaka 1948 alijigundua kuitwa katika Wito mwingine uliompelekea kujitoa maisha yake ili kusaidia watu masikini sana wa Calcutta nchini India na baadae kidogo kuanzisha Shirika la masista wa Upendo
Kwa miaka 45 alifanya kazi ya kusaidia wenye matatizo bila kuchoka na hatimae kutunukiwa Tunzo ya Amani ya Nobel mwaka 1979. Nchini India alizawadiwa Tunzo ya Bharat Ratna ambayo ni Tuzo kubwa kuliko zote nchin India katika maswala ya Utu (humanitarian).
Japokua Mama Teresa alikuja kujulikana zaidi na Shirika lake la masista wa upendo miaka 7 baada ya kifo chake baaada ya papa John Paul II baada ya kumtangaza mwenye heri. Papa ambae ni kiongozi Mkuu wa kanisa katoliki Duniani alimwelezea kama ni mfano uliokamilika wa upendo wa Mungu kwakua aliishi maisha yake kama alivyofanya Yesu kwa kuwasaidia wenye shida.
Ukitaka kujua Upendo wa Shirika alilolianzisha Tembele Kituo cha masista wa upendo pale Mburahati.
R.I.P MAMA TEREZA

<<<<<>>>
EDO DANIEL

2 comments:

  1. Thanx Joy kwa yote
    I didnt know if this story could reach tHis far
    With love
    Edo

    ReplyDelete
  2. ASANTE NAWE PIA EDO, MBONA STORY ZAKO NYINGI TU HUWA NAZIWEKA?...UZIDI KUBARIKIWA MY NDUGU.
    WITH LOVE.

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...