Social Icons

Thursday, May 16, 2013

MAYAI FEKI YASAMBAA DAR ES SALAAM


Yanatoka nchi jirani, yatengenezwa kwa umeme
Makala na Denis Mtima na Chande Abdallah
Ripoti ya Wiki hii imegundua kuwa asilimia kubwa ya mayai yanayotumiwa na wananchi wengi kwa sasa ni feki  na yanauzwa kinyemela ndani ya Jiji la Dar.

Baada ya kupigwa vita na serikali miezi michache iliyopita, imebainika kuwa bado yamezagaa na watu wanaotajwa kuyatumia kwa kiasi kikubwa ni wauza chipsi mitaani.
Mayai hayo ambayo hayatofautiani na mayai ya kuku wa kizungu yaliyozoeleka kwa kuwa na muonekano wa rangi nyeupe sana, imebainika kuwa yanatengenezwa kwa kutumia mashine maalum za umeme.

Ili kubaini uwepo wa mayai hayo ambayo serikali kupitia Bodi ya Chakula na Dawa (TFDA), iliwatahadharisha wananchi kutotumia kwa madai kuwa yana madhara kiafya, cha kushangaza bado yamezagaa mitaani kama njugu.
Ripoti ya Wiki imejaribu kufanya utafiti wa kina na kugundua uwepo wa mayai hayo hasa katika maeneo ya Buguruni na Sinza, Dar ambapo ilidaiwa kuwa mzigo mkubwa wa mayai hayo ulitokea nchini Kenya.

Aidha, kuanza kuuzwa tena kwa mayai hayo siku za hivi karibuni, kunatokana na wakazi wa jiji kutojali aina ya vyakula wanavyokula, jambo linalotoa mwanya kwa wachuuzi hao kuyapenyeza mayai hayo kwa siri kwenye mzunguko wa mayai ya kawaida.
Ripoti ya Wiki ilizungumza na mmoja wa wauza chipsi waliokutwa na mayai hayo ambaye alikiri uwepo wa mayai hayo na kubainisha kuwa yanasambazwa na wauzaji wakubwa ambao wanasemekana kuwa waliyanunua kwa wingi kabla serikali haijayapiga marufuku.

"Haya mayai mbona yapo mengi tu. Sinza nzima, ukiuliza unayapata. Watu wengi wanayakataa. Ambao hawayajui tunawabambikizia wanakula," alisema muuza chipsi huyo kwa sharti la kutotajwa jina.

Chanzo: GPL


No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...