Social Icons

Friday, October 21, 2011

JIPE MOYO WEMA SEPETU

Wema na Diamond enzi za mapenzi yao
Diamond ametamka rasmi kumuacha wema mbele ya waandishi wa habari....Maoni yangu binafsi kuhusu Wema ...Simlaumu kwa bahati mbaya anazokutana nazo kila anapokua katika mapenzi kwani mara nyingi yeye huonyesha mapenzi ya dhati aliyonayo kwa wanaume anaokua nao ilhali wao wanamchukulia kujifaidisha na pia kumtumia kwa kujiongezea umaarufu.

Wema kama nikipewa nafasi kukushauri nitakwambia tulia mdg wangu u r still young and very beutiful...Only God will give u the best husband u've never expected.Kingine achana kabisa na mapenzi na hawa wanaojiita maarufu maana siku zote wamekua watu wasiothamini penzi lako la dhati unalowapa.
Wema (Wa kwanza kushoto) akiwa na marafiki zake Lulu na Kajala
Nimeumizwa na hili la Diamond sana mpaka nimeamua kuzungumza kwani uliamua kujitoa hasa kumpenda mtu kama yeye ukajishusha pamoja na urembo wako ukajiweka sawa na yeye ukampenda kwa mapenzi yako yote lakini mwisho wake amekuacha tena kwa kashfa.
Wema siku alipovikwa pete ya uchumba na Diamond
Anza maisha yako upya mdogo wangu amini unaweza bila kuwa na hao wanaume na wala usijisikie vibaya mambo kama hayo huwapata wasichana wengi sana tofauti ni kwamba wewe ni maarufu sana so yenu yataandikwa na kusemwa sana na watu lakini usivunjike moyo kwani kila jambo huja na kupita.
Nakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya bila Diamond ...Acha kulia futa machozi simama imara jipiganie amini kwamba yupo wako atakaekupenda kwa dhati na atakaekua tayari kulinda heshima yako kwa gharama yoyote.
Diamond na Wema wapekuwa wapenzi kwa kipindi kirefu kidogo huku wakiwa na ndoto ya kuishi pamoja kama mume na mke ambapo ni takribani wiki mbili zilizopita Diamond alimvisha pete ya uchumba.

Picha na Global Publishers(Uwazi)

5 comments:

 1. Inasikitisha sana ila ndio ishatokea cha muhimu ni kujipanga upya na kuanza maisha mapya ya bila Diamond. Akitulia atapata wa kuwa nae maishani aache tabia ya kuchagua masupastaa.

  ReplyDelete
 2. UYUBEMU ATAKUA NA GUNDU KAMA SIO MABALAA KILA SIKU YEYE TUU AYA NGOJA TUONE ATATOKA NA NANI TENA BAADA YA DAIMOND

  ReplyDelete
 3. wewe anony hapo juu acha kumwambia mwenzio anagundu anauamuzi wa kugawa atakavyo kwani nani kakuambia kinaishaga

  ReplyDelete
 4. walokole feki utawajua tu
  Nyambafuuuuu

  ReplyDelete
 5. pole sio riziki yako Wema.. Tulia tafakari na vuta subira. atakaka wako tu.

  ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...