Social Icons

Friday, October 21, 2011

MATEMBEZI YA HISANI - PINK WALKATHON on Sunday 23-October-2011

MATEMBEZI YA HISANI - PINK WALKATHON 23-October-2011 (Jumapili), viwanja vya Mnazi Mmoja
Kina-mama tujumuike sote pamoja kwenye matembezi ya kilomita 5 ya pink Walkathon ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenzetu ambao tayari ni wagonjwa wa saratani ya matiti, na pia kuhamsisha wanawake kuelewa zaidi juu ya saratani ya matiti.

Fomu za Usajili kwa ajili ya matembezi zinapatikana:-

1    - Mlimani City
2.  - LAPF Millennium Tower
3.  - Shoppers Plaza (Mikocheni na Masaki)
 4.Office za TBCF, Mwananyamala Komakoma jengo la Akiba Commercial Bank au piga simu hizi kwa maelezo zaidi +255 22 2762015-17, ukishajisali utapata t-shirt

Registration fee:
Watu wazima – Inaanzia Tshs. 10000 lakini unaweza kuchangia zaidi 
Watoto – (miaka 8-15) ni Tshs. 5000/=

Wazazi wanaweza kuja na watoto wao wadogo na waangalizi wakati wazazi wanakwenda matembezini ya 5km kutakuwa na michezo mbalimbali ya watoto kama vile jumping castle nk.

Wewe uliyesoma hapa na ukaelewa nenda kawahamasishe kina mama wenzako!

Tembelea tovuti ya TBCF ingia humu www.tzbreastcancer.org
No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...