Social Icons

Tuesday, December 13, 2011

WASIFU WA MAREHEMU USIO WA KINAFIKI

Mwenyekiti wa kamati ya mazishi akainuka na kuanza kusema ‘kinachofuata sasa ndugu wafiwa na marafiki wa marehemu ni kusoma historia fupi ya marehemu tuliyemzika hapa leo, karibu ndugu uliyeandaliwa kwa shughuli hiyo’Msomaji aliyeandaliwa alianza kusoma ‘Ifuatayo ni historia fupi ya marehemu tuliyemlaza ktk nyumba ya milele.
Marehemu alizaliwa juu ya mti amb...apo mzazi wake alijihifadhi baada ya kukimbia mafuriko miaka 26 iliyopita. Hakubahatika kupata kazi ya maana japo alisoma mpaka kidato cha tano, aliamua kuacha shule mwaka juzi baada ya kuona elimu haina mpango kwake. Marehemu alikuwa kero kwa familia yake hasa kwa tabia yake chafu ya udokozi wa mboga, uongo, uvutaji bangi, ubakaji wa mifugo na baadae ushoga.


Mimi binafsi mjomba wake nimefurahishwa sana na kifo cha marehemu huyu kwani alishawahi kunipakazia kuwa nimekufa mara mbili kiasi na kufanya ndugu wote wakakusanyika na kunililia msiba.


Mtoto alitutia hasara sana kwani alikuwa mwizi wa vitu vya ndani na pesa! pia tumepoteza gharama kibao kumsomesha lakini aliishia kuwa shoga tangu tarehe 06/04/99.
Marehemu hakuugua bali kifo chake ni cha kujitakia kwani kajiua baada ya kukosa nauli ya kwenda Mombasa kuhudhuria onyesho la vikundi vitatu vya mduara.

Kwa niaba ya familia, wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu tunatoa pongezi za dhati kwa Mwenyezi Mungu kwa kutupunguzia kero na asiilaze roho ya marehemu peponi wala asimpumzishe, kama kuna mkong'oto huko ampe kiaina'.


AMINA

Thanks to Ester Ulaya Cuthbert on her Facebook wall...

3 comments:

  1. hahahhahaaaa nimecheka mie duh Ester we mkaliii

    ReplyDelete
  2. uwiii marehem ndo sifa zote hizo zake naona wangeita taarabu waserebuke hakuna kulia msibani

    ReplyDelete
  3. hunishindi mimi nilicheka, nikakohoa nikasimama, am still laughing till now

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...