Social Icons

Tuesday, January 24, 2012

Wimbo wa Leo - Majaribu wa Bahati Bukuku


Kama ilivyo ada siku ya Jumanne tunakua na kipengele cha wimbo wa leo ambapo wewe msomaji na mfuatiliaji wa Majoy Blog unaruhusiwa kuchagua wimbo wowote uupendao na kuu-dedicate kwa watu uwapendao. Ila wapendwa wangu mpo kimya sana sijapata hata email ya mtu au hakuna muwapendao?? Mimi leo nimechagua wimbo wa Bahati Bukuku uitwao MAJARIBU.

Nina sababu nyingi sana za kuchagua wimbo huo ila kikubwa ni kuwakumbusha wale wote ambao sikuzote wamekua watu wa kukata tamaa kwamba Mungu yupo na anafanya kazi mchana na usiku kuwapigania wamtumainiao.
Hivyo basi mpendwa wa Majoy Blog jipe moyo usikate tamaa kumbuka hakuna Nabii ambae hakujaribiwa maandiko yanasema wote walijaribiwa lakini walisimama na Mungu aliwashindia vivyo hivyo na wewe pia mdau wangu usiogope wala kufadhaika unapopitia katika majaribu,Bwana atakushindia kama alivyowashindia wana wa Israel kwenye bahari ya shamu atakushindia na wewe pia.

Nawatakia siku njema yenye mafanikio katika kila mtendalo. Kuchagua wimbo tuma email kwa majoy28@gmail.com


No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...