Social Icons

Thursday, June 21, 2012

MASHABIKI WOTE WA MAREHEMU KANUMBABado mpaka sasa kumbukumbu za watanzania hazijalala, movie star marehemu Steven Kanumba bado anakumbukwa kwa sababu bado kazi zake nyingi alizozifanya zinaendelea kuonekana katika maisha ya kila siku ya watanzania wengi.
Wakati huu ambapo maonyesho ya sabasaba yanakaribia kuanza Dar es salaam familia yake imeamua kuchukua banda maalum kwenye viwanja vya saba saba kwa ajili tu ya kuendelea kumuenzi Marehemu Kanumba.
Seth ambae ni Mdogo wake waliekua wakiishi pamoja Sinza Dar es salaam amesema ni banda la Kanumba litakalokua na Nguo zenye alama alizokua anazitumia Kanumba ikiwa ni pamoja na jina na ujumbe, kutakua na picha zilizo kwenye frame za Kanumba zinazomuonyesha toka akiwa utotoni, pia vikombe, kanga, bazee na vitu vingine vingi vyenye alama na picha za Kanumba.
Seth amesema Mama mzazi wa Kanumba pamoja na watu aliokua akifanya nao kazi Kanumba watakuwepo kutoa maelezo mbalimbali kuhusu Kanumba na kazi zake.
Source: Millard Ayo

No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...