Social Icons

Sunday, July 22, 2012

MAMBO 7 MUHIMU MBAYO MSICHANA/MWANAMKE UNAPASWA KUYAJUA KUTOKA KWA MWANAUME...

Edo Daniel ndiye aliyetushirikisha somo hili,fuatilia mpaka mwisho ujue ni nini kimezungumziwa hapa.
1. MWIKO: 
usithubutu kuzungumzi sifa za mpenzi wako wa zamani pindi unapoingia katika mahusiano mapya.. hii inamaanisha hauko happy na mahusiano yako ya sasa.. au unataka mwanaume huyu akufanyie yale uliyofanyiwa kule ulikotoka..... 

2. KUPIKA NI MUHIMU: 

Kujua kupika kunakuongezea mvuto kwa yule umpendae.. restaurants, takeaways and dinner out everyday? hakuna kitu kama hicho.... mfanye mpenzi wako atamani kurudi nyumbani mapema kwakuwa chakula unachopika girlfriend wake ni kitamu kuliko chakula kingine chochote

3. WORKOUT:

Hakuna mwanaume anapenda mwanamke mzembe... jitahidi kufanya mazoezi na kuhakikisha mwili wako uko katika standard.. sio wote mnauwezo wa kuingia Gym lakini jitahidi hata kukimbia kidogo uamkapo asubuhi ili kuufanya mwili wako kuwa sharp.

4.UENDESHAJI GARI
 

Wanaume hatupendi kukosolewa... hivyo basi jitahidi kuliepuka hilo au lifanye kwa busara....

5. USIVUTE SIGARA: 

Wanawake wengi huwa wanajidanganya kuwa akivuta sigara ataonekana sexy na mwenye mvuto.... huku ni kujidanganya.. utaishia kuwa katika mahusiano na masharobaro na hutaweza kupata mwanaume wa maana.. wanaume tu kuvuta sigara wanajikaza... iweje wewe mwanamke uvute??


6. KUWA WAZI NA HISIA ZAKO:
Namaanisha kuwa unapokuwa unahamu na mwenzi wako.. mweleze usiwe mtumwa wa mapenzi kwakuwa wewe ni mwanamke.. mbona Yeye anakueleza pale anapokuwa na hamu na wewe? kwanini wewe usimweleze?? unapokuwa na hamu na mzee mueleze.

7. SHORTCUTS: 

Simaanishi njia ya kukatisha ila majibu ya shortcut kama "WHATEVER","Fine", "cool" and "As u Wish" "k" hakuna mwanaume anaependa majibu kama hayo.. if u love that man why umpe majibu ya shortcut??

WENYE MASIKIO NA WASIKIE...



SHUKRANI KWA EDO DANIEL KWA HISANI YA  www.mvutokwanza.blogspot.co

No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...