Social Icons

Thursday, March 14, 2013

PAPA MPYA APATIKANA-VATICAN


Ni Kadinali Jorge Mario Bergoglio
Amezaliwa December 17, 1936 (age 76), Buenos Aires Nchini Argentina
 
Ni padre wa shirika la Majesuit akipata elimu yake katika chuo kikuu cha Buenos Aires
Kabla ya kuchaguliwa leo kua Papa alikua askofu mkuu wa Buenos Aires tangu mwaka 1998 na mwaka 2001 aliteuliwa kua Kadinali na Papa John Paul II.
 
Ni papa wa Kwanza kutoka bara ambalo lina aminika kuwa na waumini wengi wa Kanisa Katoliki (Latin America) akichagua jina la Francis I akifata mfano wa Mtakatifu Francis wa Asis mwanzilishi wa shirika la watawa wakapuchini.
Papa Francis amechaguliwa kufatia kujiuzulu wadhifa wa upapa kwa aliyekua Mtangulizi wake Papa Benedict XVI ambapo habari zinasema kua Papa huyu alishika nafasi ya Pili mwaka 2005 wakati Papa Benedict alipochaguliwa.
 
Mungu mbariki Papa Francis I!!!!
Mungu libariki Kanisa Katoliki!!!
Mungu Ubariki Ukristo wetu!!!!
 
CHANZO:

No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...