Social Icons

Wednesday, July 27, 2011

Housegirl atoroka na mtoto wa Tajiri yake!

Wapendwa,Baada ya kushuhudia kisa hiki kilichompata mfanyakazi mwenzangu, nikaona ni vyema kuwa alart wengine wenu ambao mna watoto wadogo.
Jana majira ya mchana hivi dada mmoja nafanya nae kazi alipigiwa simu kutoka Chalinze kituo cha polisi akaulizwa kama ana mtoto anayeitwa Brian na kama ana msichana wa kazi
wakataja jina lake. Dada akajibu ni kweli akaambiwa sasa hawa watu wako hapa kituoni wameletwa na konda wa basi lililokuwa linaelekea Nairobi.
Kisa chenyewe housegirl alimfungasha mtoto wa watu kaenda nae Ubungo kapanda basi, sasa baadae konda akawa anapita kukagua tiketi nadhani,sasa housegirl hana ticket akaulizwa nauli yako dada...hana..mh dada unapandaje gari huna nauli...
hana majibu....wakamuuliza unaelekea wapi...akasema anampeleka mtoto shule huko Nairobi ametumwa na wazazi wa mtoto (mtoto ana kama miaka 3-4).
Naona hapo konda wakaona kunalo jambo, so walichofanya walimpeleka kituo cha polisi cha Chalinze akatoe maelezo zaidi. Alipobanwa ndo akatoa maelezo ya mwajiri wake na namba za simu polisi wakampigia huyu dada.Dada kampata mtoto lakini bado ana shughuli ya kutoa maelezo polisi na mambo kama hayo wakati housegirl kashikiliwa na polisi. Wazazi sijui mtumie mbinu gani za kuhakikisha usalama wa watoto wenu..!

Mungu atusaidie..!

Special Thanks:

Miss Elizabeth Gervas Mtegwa,

Research and Development Officer,
Tanzania Industrial Research and Development Organization,

2 comments:

  1. Uzuri wa dunia ni kuwa na mbigu na ardhi vitu viwili vilivyo tofauti kabisa, wakati wengine wanatupa watoto wapo wanaoiba. La muhim Joy mchunge sana Derric tusije tukaonana ...

    ReplyDelete
  2. Mojaone asante kwa ushauri

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...