Social Icons

Monday, September 12, 2011

Mahusiano

Habari za week end wadau wa majoy blog...ni matumaini yangu wote hatujambo.Ningependa kuchukua fursa hii kuwapa pole wale wote ambao wamefikwa mija kwa moja na msiba uliotokana na ajali ya kuzama kwa meli huko visiwani.Tupo pamoja katika majonzi na kuwaombea kwa Mungu roho zao zipumzishwe kwa amani.Amina
Pamoja na hayo maisha yetu ya kila siku bado yanaendelea na leo tupo kwenye mada ya mahusiano ikiletwa kwenu na Daktari wa Mapenzi. Ungana nami tujue leo ana lipi la kutuhabarisha.ni matumaini yangu utajifunza kitu.....


Sababu za Kusaliti  Penzi / Pendo

*Kutopata mapenzi ya kweli hasa ikiwa Kijana/Binti alilazimishwa kuoa/kuolewa na mtu ambaye hakumpenda “for the sake of Radhi ya Wazazi”, maadili, kuhofia umri n.k..
*Uchafu, kutojijali au kujipenda.-Wote mwanaumena mwanake.
*Kutoridhika au kutosheka na wakati mwingine uroho tu- Wanaume zaidi.
*Mmoja wenu kuwa na shughuli nyingi za kikazi/Biashara, kusafiri – Wote mwanamke na mwanaume..
*Tamaa ya kumiliki vitu Fulani –Wanawake zaidi.
*Kujaribu na kujifunza mambo mapya/mitindo lakini kutokana kufuata maadili unaogopa kuwa wazi kwa mpenzi wako-Wake kwa waume..
*Kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu ikiwa mwanamke ana Mimba kubwa /amejifungua n.k-Wanaume.

Shukrani kwa Daktari Wa Mapenzi.

No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...