Social Icons

Thursday, November 10, 2011

USWAHILINI KUNA VITUKOOO

Naanza kwa kusema kuwa uswahilini kuna vituko si haba maana kwa sisi tunaoishi mitaa hiyo tunakutana na mengi yanayofurahisha na kuhuzunisha.

Kuna kisa cha aina yake kilitokea juzikati katika mitaa ya Tandale Kwatumbo, jijini Dar ambapo akina mama wa mtaa huo waliingia gharama ya kukodi Matarumbeta kwa ajili ya kumsuta mwenzao ambaye walidai kuwa ni mbeya anayewagombanisha majirani kila kukicha.

Wakati akinamama hao wakiwa wanaserebuka na matarumbeta kwa furaha kama vile wanamcheza mwari wa Kizaramo, mwana mama mmoja alisikika akimwambia mwenzie, “Mwenzangu tushachoshwa na umbeya wake yaani katugombanisha majirani wote na kasababisha Mama Wahida aachike kwa mumewe, huyu hata siyo mtu mzuri acha tumkomeshe.”
Mimi kama mwandishi nisiyepitwa na jambo nilinusanusa na kufika hapo nikawa mmojawapo wa wahudhuriaji wa shughuli hiyo, nilipopata mwanya na kumuuliza jirani mmoja kulikoni? ndipo aliponiambia kuwa kuna mama mmoja maarufu kwa jina la Mama Furaha, Tangu ahamie maeneo hayo amekuwa kero kwa majirani zake kutokana na tabia yake ya umbeya uliokithiri, hivyo wamemfungia kazi na mpaka muda huo alikuwa kajifungia chumbani kwake.

Mpaka tunakwenda mitamboni inasemekana kuwa Mama Furaha alihama kwa kutoroka usiku, vyombo vyake aliviacha, walikuja kuvichukua ndugu zake siku ya tatu.

Shukrani: GPL

1 comment:

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...