Social Icons

Friday, December 23, 2011

USED CAR IN DUBAI

STORY NA PICHA TOKA KWA MDAU NAMBA MOJA WA MAJOY BLOG...MOJAONE KUTOKA MUSCUT.

Kwa muda mrefu Dubai imekua maarufu sana kwa biashara ya used car, na serekali ya Dubai imefungua sehemu maalumu kwa kazi hiyo, nilipata bahati ya kutembelea kijiji hicho baada ya jamaa yangu mmoja toka TZ kuniomba nimtafutie FUSO.

Nilipofika sehemu hiyo nilishanga sana kuona uwingi wa magari ambayo yalipangwa kutokana na aina zake kama nyanya sokoni, kwa kuwa nilikuwa natafuta FUSO nilienda katika kona ya MAFUSO na mambo kama unavyooyaona ktk picha hizo. Kizuri zaidi ni utaratibu uliowekwa na serekali kwani ofice zote ziko sehemu moja kwa hiyo unamaliza mambo yako yote sehemu moja.
Cheki Fuso zilivyopangwa

Hii ndio niliyomchagulia jamaa yangu

Na baada ya kuzunguka kwa muda mrefu kutafuta FUSO (kutokana na wingi wa magari sio uchache, labda hii labda ile nilipata FUSO niliyoipenda nikamcukulia jamaa yangu, na nilimtembelea baada ya muda nikaikuta ikichapa kazi na kaipa jina la MA YOUNG BROTHER.


Naweza kukusaidia hata ww kupata gari yoyote uipendayo toka hapa Dubai.Kwa yeyote atakaehitaji nipo tayari kumsaidia wasiliana na Majoy anajua jinsi ya kunipata.


Nawatakia Sikukuu Njema na Kheri ya Mwaka Mpya...2012.

MOJAONE.Hapo ikiwa kazini

No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...