Social Icons

Thursday, January 19, 2012

Mkongwe wa Filamu za Kinaijeria Anusurika Kufa Kwa Ajali ya Gari

Msanii maarufu wa filamu nchini Naijeria Richard Mofe Damijo(RMD) ambae pia ni kamishna wa Utamaduni na Utalii wa jimbo la Delta amenurusika kufa baada ya gari aliyokua akitembelea kupinduka maeneo ya Warri jimboni Delta.

Ajali hiyo imefanya gari yake aina ya SUV kuharibika vibaya kama inayoonekana pichani.Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema dereva wake anahali mbaya sana hospitali. RMD aliokolewa kwenye gari hiyo baada ya ajali na kufikishwa hospitalini kwa matibabu na kwamba hali yake inaendelea vizuri.


Majoy Blog inatoa pole na kumuombea RMD na dereva wake uponywaji wa haraka ili warejee kwenye majukumu yao ya kila siku.

Shukrani kwa Adeola Adeyamo wa Naijeria kwa habari na picha.

3 comments:

  1. kweli kama zako hazijatimia hata iweje hufi.kwa jinsi hiyo gari ilivyo na watu ni wazima kweli ashukuliwe bwana Mungu.Asante Majoy kwa habari nampendaga sanapasta Ken

    ReplyDelete
  2. God is great quick recovery to all in Jesus name

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...