Social Icons

Friday, March 16, 2012

Jikoni Wikend hii......Chapati ya maji(Pan Cake)


Wikiendi hiyoooo inakuja, wafurahishe familia yako kwa kuwapikia kitafunwa hiki kitamu sana kuliwa na kinywaji chochote ,iwe chai,juice,soda au hata uji!!
Fuata maelekezo yafuatayo kwa kuandaa:.........

Mahitaji

Unga wa ngano (plain flour) 1/4

Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1

Yai (egg) 1

Chumvi (salt)

Mafuta (cooking oil)
(Waweza kuongeza kipimo kulingana na idadi ya walaji)

Matayarisho

Tia unga, chumvi na maji kiasi katika bakuli kisha koroga mpaka madonge yote yaondoke. Baada ya hapo tia yai na vitunguu kisha koroga tena mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. baada ya hapo choma chapati zako kama kawaida  na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Waweza kula kwa rost ya maini,nyama ya ng'ombe au kuku au hata mboga za majani.
 
Kila la kheri!
 
 

1 comment:

  1. kitu cha chapati rost maini na juice ya embe!!

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...