Social Icons

Friday, March 9, 2012

Mapishi ya Mchuzi wa kambaleMahitaji

Kambale 2

Nazi kopo 1

Nyanya kopo 1

Vitunguu 2

Curry powder 1 kijiko cha chai

Turmaric 1/2 kijiko cha chai

Binzari nyembamba ya unga 1/2 kijiko cha chai

Swaum/ tangawizi 1 kijiko cha chakula

Giligilani kiasi

Limao 1/2

Chumvi

Olive oil

Matayarisho

Loweka samaki katika maji ya moto kwa muda wa muda wa nusu saa.Baada ya hapo Saga pamoja nyanya, vitunguu, swaum na tangawizi kisha vibandike jikoni na uvipike mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta. Pika mpaka nyanya zitengane na mafuta kisha tia spice zote.Zipike kwa muda mdogo kisha tia tui la nazi, maji kiasi, samaki, pilipili nzima, chumvi na kamulia limao. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na samaki pia wawe wameiva na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo ipua kisha tia giligilani iliyokatwa na mchuzi utakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuulia kwa chochote kile upendacho. Mi hupendaga kuulia na ugali mlaiiini au na wali pia.
Kila la kheri najua utaenjoy waweza piga piga ukishapika na kunitumia kupitia majoy28@gmail.com
 
Tujifunze Pamojah,
 
Nawapenda sana.
 
Majoy

3 comments:

  1. Hivi Majoyy unataka nije speed kukudai huo msosi, yaani kambale ni watamuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  2. hahahhaaaa poleeee mwenyewe nimetamaniii ngoja niwatafute nikiwapata nitakuchukulia na wewe maana cjawaona siku nyingi sana

    ReplyDelete
  3. dah yani natamani nichukue ugali nile kwa picha ka mpare

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...