Bi Hawa Ngulume enzi za uahai wake. |
Bi Hawa Ngulume, aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Bagamoyo na Mbarali, amefariki dunia jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Mama Ngulume amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa kwa kipindi kirefu na mauti yamemfika akiwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar.
Kwa kujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa kamili itatolewa hapo baadaye.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMINA
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment
Thank you for your comment