Social Icons

Tuesday, December 31, 2013

MAOMBI YANAHITAJIKA KWA NYOTA HUYU WA MUZIKI WA INJILI DUNIANI


Wapenzi wa muziki wa injili duniani wameombwa kumuweka katika maombi mwimbaji nyota wa muziki wa injili Darlene Zschech ambaye amegunduliwa kuwa na kansa ya matiti mapema mwaka huu hali iliyomfanya awekwe chini ya uangalizi wa daktari siku chache kabla ya sikukuu ya krismasi.

Katika taarifa aliyotoa katika tovuti yake mwimbaji huyo ambaye alikuwa kiongozi wa sifa na kuabudu wa kanisa la Hillsong akirekodi nao matoleo mbalimbali kabla ya kustaafu na mumewe Mark na kuanzisha huduma yao, aligunduliwa kuwa na kansa ya titi tarehe 11 mwezi huu hali iliyofanya awe chini ya uangalizi wa madaktari akitakiwa kwenda kufanyiwa upasuaji na kuhudhuria kliniki ili kudhibiti kansa hiyo.


Kwa mujibu wa Darlene ambaye yeye na mumewe ni wachungaji viongozi wa kanisa la Hope UC lililopo Australia alirudi kutoka hospitalini usiku wa kuamkia krismasi na kuweza kuangalia ibada ya usiku mtakatifu ya kanisa lake kwa njia ya mtandao na kufurahishwa jinsi watenda kazi pamoja naye walivyofanya kazi njema usiku huo. Mwanamama huyo amesema kuwa licha ya kwamba anapitia kipindi kigumu wakati huu lakini anashukuru Roho mtakatifu na neno la Mungu ambalo linamtia nguvu ya kusonga mbele, huku akimshukuru mumewe na watoto pamoja na waimbaji wenzake ndugu jamaa na marafiki ambao wamekuwa naye bega kwa bega wakimuombea ikiwa pamoja na kupakwa mafuta na viongozi wa kanisa lake analolichungawakimuombea kwa mzigo.

Aidha Darlene amesema habari hii si aina ya habari ambayo watu wangependa kusimulia lakini amesema ameona miujiza miwili ikitendeka katika mwili wake na kuendelea kuamini kwamba kuna mingine zaidi itaendelea kutendeka. Zaidi mwanamama huyo amewashukuru daktari wake wa upasuaji, manesi wa hospitali ya SAN pamoja na Central Coast APAC ambao wameonyesha kumjali sana kwa huduma yao. Darlene amesema pamoja na hayo yote moyo wake umejawa na pendo kuu la Mungu akiachia kitabu cha Zaburi 1, Waefeso 3, Yeremia 30, Zaburi 66;12 pamoja na mistari mingine ya Biblia.
Darlene ameshiriki kikamilifu katika kanisa la Hillsong na kufanyika kama nembo ya band ya kanisa hilo kwa zaidi ya miaka 20 hadi alipoamua kukaa pembeni na mumewe miaka mitatu iliyopita na kuanzisha kanisa lao ambalo limeendelea kukua siku kwa siku. Kati ya nyimbo nyingi alizowahi kutunga ama kuimba wimbo "Shout to the Lord" ndio wimbo uliomtambulisha zaidi. Angalia wimbo huu chini akiwa amemshirikisha Michale W. Smith.Mkumbuke Darlene Zschech Mungu akatende jambo juu ya mtumishi wake huyu.

Chanzo: Gospel Kitaa na HAPA


No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...