Mdada akila majani ambayo huduma hiyo wanasema ni chakula kutoka mbinguni mwe!
|
Kuna mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu huduma za watumishi mbalimbali,
moja wapo ni hii huduma iitwayo Rabboni Centre ministries iliyopo Pretoria nchini Afrika ya kusini, huduma hii iliyochini ya mwanzilishi wake mwalimu ,mchungaji na nabii Daniel Lesego ilianza mwaka 2002.
Ni huduma ambayo kwa watu wasioabudu hapo huitilia mashaka kutokana na mwenendo wake.
Ni huduma ambayo kwa watu wasioabudu hapo huitilia mashaka kutokana na mwenendo wake.
Kwasasa wapo kwenye mfungo ambao watu hufika kanisani na hatimaye wanaishia kula majani
yaliyopo nje ya kanisa hilo akisema kwamba Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote huku
ikidaiwa kuwa manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.
Inaelezwa kwamba mara baada ya maombi waumini wengi huanza kutapika jambo
ambalo kanisani hapo huashiria kwamba mtu amejazwa Roho Mtakatifu.
Lakini kama haitoshi nabii Lesego hufanya maombi huku amewakanyaga watu.
Huduma hii imekuwa gumzo nchini humo na nchi jirani kwa jinsi mambo yao yanavyokwenda.
Mnasemaje watumishi kuhusu jambo hili? mwe kula manyasi kweli? mma!
Hapa nabii huyo akikanyaga watu kama njia ya mafundisho yake. |
Haa!! angalia jamani, sasa ng'ombe watakula nini jamani??? |
Mungu tufunulie macho ya rohoni kuyajua mambo haya kama ni wewe au sisi kha! |
Hajamaliza bado. |
Baada ya manyasi ni mwendo wa kutapika sasa |
Picha ya juu na hii huyu ndio nabii Lesego Daniel mwenye maono na huduma hii. |
Watu wanajaa kwenye huduma. |
Mwe! kama uti wa mgongo shida hii dawa |
Maombi yanaendelea. |
Nabii anafundisha huku skuna yake imekanyaga mtu, sijui |
Tembelea TOVUTI YAO Picha zote kwa hisani ya ukurasa wao wa Facebook.
Chanzo: Gospel Kitaa
Wajinga ndo waliwao.wapenda miujiza watakoma
ReplyDelete