Social Icons

Wednesday, March 21, 2012

Bibi wa Miaka 105 Ajiny'onga Baada ya Kuchoka Kuishi....

Anastasia Khoreva
Mwanamke huyo kikongwe (pichani) amejinyonga mpaka kufa baada ya kuchoka kusubiri kifo akiwa na umri wa miaka 105.
Bibi huyo alipata mfadhaiko baada ya kuugua mapafu na kukaa ndani muda mrefu.Majirani zake wanadai kuwa bibi huyo alisubiri wakati watu wote wakiwa wametoka na yeye alitumia muda huyo kutimiza azma yake ya kujiny'onga.
Imedaiwa kwamba bibi huyo alishawahi kujaribu kujiua mara kadhaa bila mafanikio kwa madai kwamba amechoka kuishi.
Maoni yangu: Uhai wa mwanadamu ni zawadi toka kwa Mungu na si mali yetu hivyo basi si vizuri kuukatisha kabla Mungu hajaona vema kufanya hivyo.
Muwe na siku njema wapendwa wangu.

Majoy.

1 comment:

  1. Yuko sahihi, ni haki ya mtu kuchagua; akichoka kuishi katika umri huo ni halali yake kujitoa uhai kwa hiyari yake mwenyewe!

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...