Social Icons

Tuesday, March 6, 2012

Mapishi Ya Mboga Mchanganyiko

Muonekano wa mboga zako baada ya kuiva..yummy!!
Mahitaji

Viazi ulaya 4 vya wastani
Hoho jekundu 1/2
Hoho la njano 1/2
Hoho la kiajani 1/2
Njegere 1 kikombe cha chai
Carrot 1 kubwa
Broccoli kidogo
Cauliflower kidogo
Kitunguu 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chakula
Curry powder 1 kijiko cha chakula
Coriander powder 1 kijiko cha chai
Tarmaric 1/2 kijiko cha chai
Olive oil
Chumvi
1/4 ya limao


Matayarisho
Katika sufuria isiyoshika chini kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia swaum/tangawizi na spice zote kaanga kwa muda mfupi kisha tia nyanya na chumvi. pika mpaka nyanya ziive kisha tia vegetable zote na vimaji kidogo sana na kisha kamulia limao, baada ya hapo punguza moto na kisha funika na zipike mpaka vegetable zote ziive na rojo ibakie kidogo. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
Kila la Kheri. 
Majoy.

3 comments:

  1. Huwezi amini,kuna vitu ambavyo cjui vinafanaje hapo. km Broccoli kidogo, Cauliflower kidogo
    Curry powder,Coriander powder,Tarmaric,Olive oil. Japo weka picha kidogo ili nivitafute nami nijaribu, maana huo msoc umenivutia.

    ReplyDelete
  2. Stella asante kwa kufatilia posts zangu ...ila hivyo vitu ni vya kawaida na vinapatikana sana kwenye supermarket sehemu wanazouza viungo na mbogamboga pia ni bei poa sana.
    Vitafute upike na ututumie picha nitafurahi kuiweka kwa blog.
    Kila la kheri dia.

    ReplyDelete
  3. DU LINA MVUTO NA UGALI SIPATI PICHA MTU ANIPIKIE HILO DIKODIKO MBONA NATANGAZA NDOA

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...