Social Icons

Friday, March 23, 2012

Mkate wa mayaiMahitaji

Slice za mkate 6

Mayai 3

Chumvi

Olive oil/mafuta yoyote ya kupikia

Matayarisho

Vunja mayai yote katika sahani kisha tia chumvi kidogo sana na uyapige mpaka chumvi ichanganyike. Kisha chukua frying pan na utie vimafuta kidogo na uweke jikoni. Mafuta yakishapata moto kiasi,chovya slice za mkate katika hayo mayai na uzipike pande zote zikishaiva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili kukausha mafuta.Na baada ya hapo mikate yako itakuwa tayari kwa kuliwa na chai.

Ni nzuri pia kwa watoto,so wafurahishe familia yako kwa kuwaandalia hii kwa weekend.....

Bless u all,

Majoy.

No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...