Social Icons

Monday, May 7, 2012

MASKINI MTOTO HUYU ........
Mtoto Deus Juma (7) akiwa ameunguzwa vibaya kwa maji ya moto na mama yake baada ya kumtuhumu kumuibia shilingi 6,000. MUSWADA wa Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 ulipitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba, 2009.

Ilikuwa ni miaka 20 tangu Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto (UNCRC) upitishwe na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2009 na miaka 19 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Kimataifa wa Haki na Ustawi wa Mtoto (ACRWC) 1990.

Kutungwa kwa Sheria ya Mtoto ni matunda ya juhudi za muda mrefu za Kitaifa na Kimataifa kuona kuwa Tanzania inakuwa na Sheria mahususi ya mtoto kwa ajili ya kuendeleza na kulinda haki za mtoto Tanzania.
Pamoja na jitihada zote hizo katika kuhakikisha kwamba haki za watoto zinalindwa na kusimamiwa kikamilifu, Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wadogo bado vinaonekana kuchukua kasi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na hivyo kuwaumiza na kuwanyima watoto haki zao za msingi.Kwa habari zaidi
4 comments:

  1. DAH HURUMA SANA BINADAMU WAMEKUA WANYAMA HATA KWA MALAIKA JAMANI MUNGU APISHIE MBALI.

    ReplyDelete
  2. Yani kuna watu wana roho mbaya ka wakaanga sumu

    ReplyDelete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...