Social Icons

Thursday, July 21, 2011

KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI ASIMAMISHWA KAZI!


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo (pichani) amesimaishwa kazi! Akiongea na waandishi wa habari mjini Dodoma mapema leo, Katibu Mkuu Kiongozi, Philomon Luhanjo, alisema kuwa Jairo amesimamishwa kazi kuanzia kesho ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zilizotolewa bungeni mapema wiki hii. Jairo anatuhumiwa kuandika barua ya kuchangisha fedha milioni 50 kwa idara 20 ili zitumike kushawishi wabunge wapitishe bajeti ya wizara yake. Haijaelezwa amesimamishwa kwa muda gani.

No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...