Social Icons

Monday, October 31, 2011

YALIYOJIRI WEEK END - JUMAMOSI

Kwanza nilichelewa sana kuamka maana nililala late sana, nilipoamka nilifanya shughuli za hapa na pale ikiwemo kupika maana msaidizi wangu week end huwa anapumzika kama nikiwepo home namsaidia kuandaa chakula cha familia na yeye anafanya kazi ya kumuangalia mtoto.

Mida ya saa nane hivi nikiwa na marafiki zangu Edo,Maggie na Esher tuliondoka zetu kuelekea uwanja wa Taifa kuangalia mechi kati ya Simba SC na Yanga SC mimi na wenzangu tukiwa ni mashabiki wa ukweli wa Simba SC.
Tazama picha za matukio mbalimbali ya shangwe za kuishangilia timu yetu ya Simba SC.
Edo, Esher na Maggie

Sisi ni Simba mpaka damuniiii

Hapo wakiingia uwanjani kwa mbweeembeee kumbe twaenda pokea kipigooo!!

Jua lilitukomesha lilikua kali mno.....upenzi kazi sana

Jua lilikua kali sana lakini tumo tu ushabiki toka rohonii

Esher na shabiki mwenzetu tulimpenda tu alivyovaa

MASHABIKI WA UKWELIIIII

Simba SC timu kubwa bwana hadi watoto walivaa red kuisapoti

Esher na Mashabiki wake wa movie nao wakiwa ni mashabiki wa ukweli wa Simba SC

Mashabiki wa Simba na Majoy Blog

Ice cream time ......


Tuliondoka kwa shangwe kama hatujafungwa vileeee

Na siku hiyo ikaishia hapo kwa kila mtu kurudi makwao.....


No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...