Social Icons

Saturday, August 25, 2012

MASKINI BABU MATONYA MAY HIS SOUL R.I.P

Omba omba maarufu nchini Tanzania Matonya amefariki dunia. Paulo Mawezi (Matonya) a.k.a Rais wa Dodoma ni mmoja kati ya watu maarufu sana hapa nchini. Jina lake limetajwa sana, picha zake zimejitokeza mara nyingi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya intaneti. Wakati Yussuf Makamba akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mzee huyu alipata umaarufu kutokana na mchuano wao, anatajwa na Prof. Jay kwenye wimbo wake Bongo Dar es Salaam. Huyu ni mzee ,  R.I.P Mzee Matonya. 

 DONDOO KUHUSU MATONYA

Jina lake halisi ni Paulo Mawezi
Jina Matonya ni la utotoni
Ni mume wa wake watatu
Ni baba wa watoto wawili, Elizabeth na Ernest
Aliishi Kilimatinde, Singida miaka 30 iliyopita
Mpaka mauti yanamfika alikuwa mkazi wa Bahi Sokoni, Dodoma
Alianza 'kazi' ya ombaomba kabla ya Uhuru
Alikuwa akikusanya kati ya sh 4000 na 7000 kwa siku
Aliwahikutoroka kambini Morogoro, akapandishwa kizimbani

HABARI NA PICHA SHUKRANI FATHER KIDEVU BLOG.

No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...