Social Icons

Wednesday, September 26, 2012

TATHMINI YA MAJINA KWA KUTUMIA HERUFI ZA MWANZO ZA MAJINA HAYO

HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa,
anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye
tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda
Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.

HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda
kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anap
otaka kulinda vilivyo katika himaya yake.

HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika,
mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu
na wanaopenda mawasiliano.

HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni
watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye
msimamo.

HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi
na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na
hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.

HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho
nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni
lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.

HERUFI G
Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na
nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya
watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri
wa kutoka kwa watu.

HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika
biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye
mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.

HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana
huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.

HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu
na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati
mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.

HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo
thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu
wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali
ya kimaisha.

HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na
aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.

HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana,
mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi
kukasirika.

HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na
hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.

HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na
mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye
uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.

HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na
hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye
mambo ya watu.

HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili.
Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata
hivyo ni mtu aliyepooza sana.

HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma
lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.

HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta
utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa
kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya
muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.

HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla.
Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na
aliyekosa maamuzi.

HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie
choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.

HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita
kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa
na hufanya mambo ya hatari.

HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi
katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa
uaminifu.

HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na
hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na
husababishia kupoteza bahati katika maisha.

HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na

BY EDO DANIEL(Mfalme Edo)

6 comments:

  1. HA HAHA HA FOR SURE NAPENDA UHURU KATIKA MAPENZI..

    ReplyDelete
  2. HERUFI M
    Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana,
    mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi
    kukasirika.

    KTK KIPENGILE CHA MROPOKAJI NAKUBALIANA NAWE 100%

    ReplyDelete
  3. HERUFI S
    Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta
    utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

    HAPO UMECHEMSHA SIVYO NDIVYO KABISA

    ReplyDelete
    Replies
    1. ONE KUMBUKA HUYO ALIEANDIKA NI BINADAMU WA KAWAIDA WALA SIO MUNGU SO SIO LAZIMA KWAKO IWE SAWA,YAWEZA KUWA SIO KWAKO NA NDIO KWA MWINGINE.

      Delete

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...