Social Icons

Wednesday, March 7, 2012

Vunja Mbavu...... Rushwa Ilivyokita Mizizi!!!Padre mmoja akiwa kwenye gari alisimamishwa na Trafic Police, police akiwa anahitaji rushwa alianza kuuliza maswali mengi,mara mbona gari lako linatoa moshi mwingi? mbona gari lako matairi yameisha, hatimayepolisi akamuamuru padre waende nae kituoni.

Njiani polisi alimuuliza padre, umesema wewe ni padre, je unabiblia ndani ya gari, padre akajibu ndio ninayo, polisi akamuambia padre, pack gari pembeni na unipe biblia. Padre akapaki gari na kumpa biblia yule polisi,
Polisi akasita kupokea, akamwsambia Padre 'fungua na usome Matayo 5:25-26 "Mtu wa Mungu akasoma ": malizaneni na aliyekukamata kukupeleka mahakamani.. ..malizaneni upesi.. yamalize mambo haya mngali bado njiani kabla hajakukabidhi kwa hakimu... ambaye aweza kukuhukumu na kukukabidhi kwa bwana jela ili akutie gerezani. Amin nakwambia hautaachiwa hadi umetoa senti ya mwisho...

Mtu wa Mungu akampa yaliyo yake kaizari. Polisi akatabasamu na kusema 'msifanye migumu mioyo yenu.. nenda na amani.No comments:

Post a Comment

Thank you for your comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...